Mama kusafiri na ndege akiwa na watoto wake


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kusafiri na watoto wake kwa ndege kwa muda wa masaa matatu?

Jibu: Ikiwa watoto wake ni wakiume na wameshabaleghe, hakuna neno. Mvulana ambaye kishabaleghe anakuwa ni Mahram. Ikiwa miongoni mwao kuko ambaye kishabaleghe na ana akili, anakuwa ni Mahram wake. Ama ikiwa bado ni wadogo na hawajabaleghe, si sawa na hawawezi kuwa Mahram wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (68) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13864
  • Imechapishwa: 16/11/2014