Swali: Kuna mtu amezikwa na hazina. Je, inajuzu kufukua kaburi na kutoa hazina hiyo pamoja na kuzingatia kuwa mtawala katika nchi yetu anakataza ufukuaji wa sampuli hii?

Jibu: Ikiwa maiti amezikwa na mali lifukuliwe na mali hiyo itolewe. Haijuzu kuharibu pesa. Haimnufaishi kitu maiti. Kwa vile haifai kuharibu mali, kitendo hichi kinajuzu ikiwa hakutotokea matatizo yoyote. Ikiwa kutatokea matatizo iacheni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%204%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 13/03/2017