Malengo ya chimbuko la neno ”wakristo”

Swali: Je, inajuzu kuwaita manaswara ´wakristo`?

Jibu: Hili ni jina lililozoeleka hii leo. Allaah amewaita katika Qur-aan ´manaswara`. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaita ´manaswara`. Wanachuoni wa waislamu wamewaita ´manaswara`. Hali iliendelea hivo mpaka punde tu wakati ambapo manaswara walipoenda kukoloni baadhi ya miji ya Kiislamu ndipo wakasema ya kwamba sisi ni wafuasi wa Muhammad na wao eti ni wakristo (مسيحيون). Malengo yao ni kutaka umoja kati ya waislamu na manaswara.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/682
  • Imechapishwa: 18/10/2017