Swali: Inajuzu kuswali nyuma ya mnyoa ndevu? Ni ipi hukumu ya kunyoa sehemu ya ndevu kwa mfano za kwenye mashavu?

Jibu: Kama ni imamu haitakikani kumfanya imamu akiwa ni mnyoaji, mtu wa Bid´ah au mtenda maasi. Watu kama hawa haitakikani kuwafanya maimamu. Maimamu wanatakiwa kutafutwa watu wenye kheri na wema. Lakini endapo watu watapewa mtihani na yeye mtu huyo akawa ndiye imamu wa msikiti basi kuswaliwe nyuma yake na swalah ni sahihi kwa mujibu wa maoni yenye nguvu miongoni mwa maoni ya wanachuoni. Swalah nyuma yake ni sahihi watu wakipewa mtihani kwa imamu huyo. Lakini haitakikani kumteua imamu na wala haitakikani kumkubalia. Bali inapaswa kujitahidi kumng´oa na kumuweka nafasi yake ni mwenye kusilihi zaidi kuliko yeye.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3701/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%AE%D9%84%D9%81-%D8%AD%D8%A7%D9%84%D9%82-%D8%A7%D9%84%D9%84%D8%AD%D9%8A%D8%A9
  • Imechapishwa: 20/02/2020