Swali: Mwanamke ambaye ni bibi kizee ni lazima awe na Mahram katika safari?

Jibu: Ndio. Hadiyth ni yenye kuenea:

“Si halali kwa mwanamke anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”[1]

Ni mamoja mwanamke huyo ni kijana au ni mzee. Hadiyth ni yenye kuenea. Haijuzu kuikhusisha isipokuwa kwa dalili kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] al-Bukhaariy (1088) na Muslim (1339).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017