Mafungu ya watu katika Tarawiyh


Swali: Nawaona waswaliji katika swalah ya Tarawiyh wakiwa mafungu yafuatayo:

1- Kuna fungu la watu linalotoka kabla ya shafa´ na Witr.

2- Kuna fungu la watu linalotoka kabla ya Witr.

3- Kuna fungu la watu – ikiwa maimamu ni wawili – linalotoka baada ya kumaliza yule imamu wa kwanza.

4- Kuna fungu la watu pale ambapo imamu anapomaliza kuswali Witr wanaswali Rakaa´ moja shafa´ juu ya ile Witr.

Tunaomba utufaidishe kwa kina juu ya maudhui haya. Ni lini mtu anazingatiwa kuwa amesimama pamoja na imamu ili aweze kupata zile thawabu zilizopokelewa katika Hadiyth? Allaah akujaze kheri.

Jibu: Yote aliyotaja muulizaji yanajuzu. Jambo hili kuna wasaa ndani yake na himdi zote ni stahiki ya Allaah. Lakini yule mwenye kubaki pamoja na imamu mpaka akamaliza ndiye anayefikia katika fadhilah na anahesabika ni kama ambaye ameswali usiku mzima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kusimama pamoja na imamu mpaka akamaliza basi ataandikiwa kama amesimama usiku mzima.”[1]

[1] at-Tirmidhiy (806), an-Nasaa´iy (1605), Abu Daawuud (1375) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/28)
  • Imechapishwa: 21/05/2018