Madhehebu Ya Salaf Juu Ya Sifa Za Allaah


Swali: Baadhi ya maduka ya vitabu masokoni yanathibitisha kuwa madhehebu ya Salaf yanasema kuwa maana na namna ya sifa za Allaah yanajua Allaah peke yake.

Jibu: Hapana. Si sahihi. Madhehebu ya Salaf yanasema kuwa namna ya sifa za Allaah inajua Allaah peke yake. Aliyesema kuwa madhehebu ya Salaf yanasema kuwa maana inajua Allaah peke yake amekosea. Bali yanasema kuwa kuwa namna ya sifa za Allaah inajua Allaah peke yake. Sisi tunajua nini maana ya Mwingi wa huruma (ar-Rahmaan), mwenye kurehemu (ar-Rahiym), maana ya Mwenye kusikia (as-Samiy´), Mwenye kuona (al-Baswiyr), maana ya Mwenye nguvu (al-´Aziyz), Mwenye kuhukumu (al-Hakiym). Lakini hata hivyo namna yake hatujui. Hatujui namna ulivyo huruma Wake, namna alivyolingana na namna ilivyo elimu Yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 08/12/2016