Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa pete ya chuma? Je, imethibiti kuwa ni pambo la watu wa Motoni?

Jibu: Imechukizwa. Imechukizwa kuvaa pete ya chuma. Lakini hata hivyo imetuhusiwa. Kwa dalili ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliposema kumwambia mwanaume yule aliyemuomba amuozeshe mwanamke baada ya kumwomba atoe mahari na hakuwa na kitu ndipo akamwambia:

“Tafuta japo pete ya chuma.”

Haya yanathibitisha kujuzu kwa pete ya chuma. Inafahamisha kuwa imechukizwa machukizo ambayo sio ya haramu. Lakini wakati wa haja machukizo yanaondoka.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 04/04/2017