Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya moto?

Jibu: Hakuna neno. Kuswali na mbele kuko moto ni jambo lenye kuchukiza. Lakini mtu akihitajia kufanya hivo basi yale machukizo yanaondoka. Kama mfano mtu anahitajia kupata joto kidogo. Vinginevyo kimsingi ni kwamba imechukizwa. Kwa sababu kufanya hivo kuna kujifananisha na majusi ambao ni waabudu moto.

Kwa hiyo jambo lenye kuchukiza ni pale moto utakuwa mbele ya yule mwenye kuswali. Ama moto ukiwa upande wake wa kulia, upande wake wa kushoto au nyuma ya mgongo wake [hakuna machukizo]. Ukiwa mbele yake basi anatakiwa kuuweka mbali hata kama utakuwa ni moto wa umeme au mwengineo. Isipokuwa ikiwa kama mtu atauhitajia. Kukiwepo na haja ya kufanya hivo basi machukizo yanaondoka.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 03/09/2018