Swadaqah katika Shari´ah haikukomeka katika mali. Swadaqah ya mali ni aina moja wapo ya swadaqah. Maana ya swadaqah ni kufikisha kheri na manufaa kwa wengine. Kwa ajili hii Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni Mwenye kusifiwa kwamba ni mwenye kutoa swadaqah kwa waja Wake, kama ilivyothibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 360
  • Imechapishwa: 14/05/2020