Maana ya mke kuwa muasi


Maana ya mke ambaye ni muasi ni kwamba anakataa haki za mume. Hata hivyo ikiwa atamkatalia kitu ambacho sio katika haki zake za wajibu, haichukuliwi kama ni muasi hata kama mke atasema kuwa ni kumuasi mume wake. Ikiwa mume atamwambia kusimama sokoni au kufanya kazi kama muuzaji mtangazaji na akawa amekataa, sio lazima kumtii. Ikiwa atamwambia kuwa mtumishi kwa watu wengine, sio lazima kwake kumtii.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumti´ (12/440)
  • Imechapishwa: 20/09/2020