Kauli hii, nayo ni ile inayosema kuwa Hadiyth-ul-Qudsiy matamshi yake yanatokana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na maana ndio yenye kutoka kwa Allaah (Jalla wa ´Alaa), inaafikiana na kauli ya Ashaa´irah, Maaturiydiyyah na mfano wa watu hawa, ya kwamba maneno ya Allaah (Jalla wa ´Alaa) ni yenye kusimama katika nafsi Yake, bi maana huweka kwenye roho ya Jibriyl au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maana na Jibriyl au Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaeleza kwa yale anayoyaona.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 360
  • Imechapishwa: 14/05/2020