Lengo la mwanamke kuwa na Mahram safarini

Swali: Je, imeshurutishwa Mahram awe tayari ameshabaleghe? Kuna mtu anafanya kazi nje ya nchi na yuko pamoja naye mke na mvulana wake ambaye ana umri wa miaka tisa. Mke akataka kuhudhuria ndoa ya kaka yake ambapo mume akamtuma kwa usafiri wa ndege akiambatana na mtoto huyu. Baada ya hapo akawasiliana na familia yake waje kumpokea katika uwanja wa ndege. Je, inafaa kwake kufanya hivo? Je, mtoto huyu anatosha katika suala la u-Mahram?

Jibu: Wanachuoni wametaja masharti mawili juu ya Mahram:

1- Kubaleghe.

2- Akili.

Wamesema kwamba ambaye bado hajabaleghe hafai kuwa Mahram. Vilevile ambaye hana akili hafai kuwa Mahram. Kwa sababu lengo la kuwa pamoja na Mahram ni kumlinda na kumhifadhi yule mke na kuzuia asije kushambuliwa. Mtoto mdogo hayawezi mambo haya. Kwa mujibu wa swali mwanamke tayari ameshafika katika mji wake. Nasema kwamba asirudi kwa mume wake mpaka mume wake huyu arudi na kumchukua pamoja naye. Vilevile anaweza kusafiri pamoja na mmoja katika Mahram zake ambao wamekwishabaleghe na kuwa na akili. Kuhusu mtoto mdogo ambaye umri wake ni wa miaka tisa hatoshi kuwa Mahram.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (47) http://binothaimeen.net/content/1084
  • Imechapishwa: 28/03/2019