Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayeenda Makkah yeye na watoto wake kutekeleza ´Umrah na akawaacha watoto wake wakazurura katika masoko na barabara ilihali yeye ameshughulishwa na ´ibaadah?

Jibu: Naona kuwa mtu huyu yuko karibu zaidi na dhambi kuliko thawabu. Kwa sababu kuwaangalia watoto na kuwalea ni jambo la wajibu zaidi kuliko kwenda ´Umrah. Bali kwenda ´Umrah ni imependekezwa tu na sio lazima. Ni vipi ataacha jambo la lazima na akafanya jambo lililopendekezwa? Ni jambo linalojulikana kwamba kumwabudu Allaah hakutokani na matamanio. Bali kunatokana na uongofu na yale yaliyofahamishwa na Shari´ah. Ama tungelifanya kila mmoja anamwabudu Allaah kwa mujibu wa matamanio yake, basi watu wangelifarikiana, wakatawanyika na wakawa aina mbalimbali.

Ni wajibu kwa mtu kuichunga familia yake. Hata tukikadiria kuwa amesafiri kwenda Makkah na akaicha familia yake basi amepata dhambi. Isipokuwa ikiwa kama atasafiri kwenda Makkah kufanya ´Umrah na akarudi siku hiyohiyo. Mtu kama huyu natarajia kuwa hapati dhambi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (70) http://binothaimeen.net/content/1602
  • Imechapishwa: 21/03/2020