Kwenda kwenye kituo kingine

Swali: Pindi mtu anapoirudi ´Umrah iliyoharibika ni lazima kwenda kwenye kituo kilekile alichohirimia au inatosha kwenda kuhirimia kutoka Tan´iym?

Jibu: Anatakiwa kwenda kwenye kituo kilekile alichohirimia kwa ´Umrah ile iliyoharibika. Anapaswa kwenda huko na ahirimie kutokea huko. Haisihi kwenda kwenye kituo kingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (21) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 07/03/2020