Swali: Unasemaje juu ya mwenye kusema: “Ni lazima somo la ´Aqiydah leo likomeke na masuala ya kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah na uanasekula kwa sababu hayo ndio yameenea katika zama hizi. Ametumia hoja kwa Da´wah ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab ya kwamba ilikuwa inahusiana tu na Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah kwa sababu ndio ambayo ilikuwa yenye kuenea katika zama zake kumshirikisha Allaah katika ´ibaadah.”?

Jibu: Ndugu! Kuhukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah ni kitu kinachoingia katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Kuhukumu kwa Shari´ah ni kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo ni kitu kinachoingia ndani yake. Sio kwa sababu kwa dhati yake yenyewe ndio Tawhiyd yote, bali ni sehemu ya Tawhiyd. Kikubwa kinachofanywa hii leo ni shirki. Ni kwa nini huyu ana papara za kukemea kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah na huku amesahau ´ibaadah za makaburi na ´ibaadah zinazofanywa kwa asiyekuwa Allaah na ´ibaadah za kuabudu mashaytwaan? Ni kwa nini anasahau haya na kuyaacha na ametilia mkazo tu kuhukumu kinyume na aliyoteremsha Allaah? Hata kama kutahukumiwa kwa Shari´ah na wakati huo huo shirki ikawa haijakatazwa halitofaa chochote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 27/04/2018