Kwanini asikufurishwe yule anyepinga sifa za Allaah?


Swali: Anayekanusha Sifa anakufuru? Ni kwa nini Salaf hawakuwakufurisha Mu´tazilah na Ashaa´irah?

Jibu: Unajuaje kama hawakuwakufurisha? Yule anayekanusha Sifa na Majina kwa Allaah, ikiwa ni mwenye kufuata kichwa mchunga au anaziwekea taawili na huku akifikiria kuwa yuko katika haki, huyu hakufurishwi. Anapewa udhuru kwa taawili au kufuata kichwa mchunga. Ama yule anayekusudia kukanusha Sifa na Majina ilihali anajua, huyu hakuna shaka yoyote ya kufuru yake.

Wanachuoni elfu khamsini – kama alivosema Ibn-ul-Qayyim – wamewakufurisha Jahmiyyah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_05.mp3
  • Imechapishwa: 30/06/2018