Kwanini asikufurishwe anayepinga jina au sifa ya Allaah?

Swali: Je, ikithibiti kuwa ´Ashaa´irah wanaipindisha maana sifa wanakufuru kwa kitendo hicho?

Jibu: Mtu kupindisha maana ya sifa hakufuru. Yule mwenye kukanusha jina miongoni mwa majina ya Allaah ndiye anakufuru. Allaah (Ta´ala) amesema:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa huruma amelingana juu ya ‘Arshi.”[1]

Akipinga jina miongoni mwa majina ya Allaah pasi na kupindisha maana ndipo anakufuru:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

“Mwingi wa huruma amelingana juu ya ‘Arshi.”[2]

Akipinga Aayah anakufuru. Lakini akipindisha maana kwa kusema “kulingana/kuwa juu” maana yake ni kutawala, anakuwa ni mwenye utata. Hakufurishwi.

[1] 20:05

[2] 20:05

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 07/09/2019