Kwanini asikufurishwe anayechukia kitu kilichoruhusiwa?

Swali: Mwenye kuchukia kitu kilichoruhusiwa au ambacho wanachuoni wametofautiana anaingia katika kichenguzi cha tano[1]?

Jibu: Mtu ana udhuru juu ya kitu kilichoruhusiwa au ambacho wanachuoni wametofautiana. Ikiwa mambo ndani yake kuna tofauti na yeye akawa amechukua moja katika wezekano nyingi au moja katika maoni fulani, huyu akiwa ni Mujtahid na anaweza kuchagua ni ipi haki anapewa udhuru, na akiwa amechagua hiyo kwa sababu yanakwenda sambamba na matamanio yake, hapana shaka kwamba ni kosa na anapata dhambi. Lakini haijafikia kiwango cha kuritadi.

[1] Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yule mwenye kuchukia kitu katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ijapokuwa atakifanya, amekufuru. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

”Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale aliyoyateremsha Allaah, basi akayaharibu matendo yao.” (47:09)

 

 

 

 

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 125
  • Imechapishwa: 24/11/2018