Kwa sababu hii kunyoa ndevu ikawa ni dhambi kubwa


Swali: Dhambi ambazo zina kujifananisha na makafiri na wanawake, kama mfano wa kunyoa ndevu, kunazingatiwa kuwa ni dhambi kubwa?

Jibu: Ni kujifananisha na wanawake. Vilevile kuna laana juu ya hili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanaume wenye kujifananisha na wanawake na amewalaani wanawake wenye kujifananisha na wanaume. Hii ni dhambi kubwa kwa ajili ya laana na sio kwa ajili ya kujifananisha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2018