Kuwapa watoto jina la Mitw´ib, Twaa Haa na Yaa Siyn


Swali: Ni ipi hukumu ya kujiita kwa majina haya; Mitw´ib, Twaa Haa na Yaa Siyn?

Jibu: Mitw´ib sio lizuri. Mtu ajiite kwa jina zuri kuliko Mitw´ib. Mitw´ib maana yake ni mwenye kuwataabisha watu.

Ama kuhusu Twaa Haa na Yaa Siyn, haya sio majina. Hizi ni herufi za mkato. Twaa Haa ni herufi za mkato. Kadhalika Yaa Siyn ni herufi za mkato ambazo zinakuwa mwanzoni mwa Suurah. Lakini watu wameyafanya kuwa ni majina ilihali sio majina. Wanadai kwamba ni katika majina ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanasema Mtume jina lake ni Twaa Haa au Yaa Siyn. Hili ni kosa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1431-5-25.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014