Kuwaleta watoto wanaoleta vurugu msikitini wakati wa swalah

Swali: Sehemu ya kuswalia kwa wanawake kunatokea mambo kadhaa ikiwa ni pamoja vilevile na kwamba baadhi ya wanawake huwaleta watoto wakiwa pamoja nao. Kutokana na ile khofu yake kubwa juu yao huenda akawaandamiza kwa kuwatazama na pengine hilo likapelekea kugeuka kiasi kikubwa. Hali inaweza kufikia mpaka akatoka nje ya swalah na yeye kwa mfano yuko katika Rakaa´ ya pili ambapo akaenda na kumleta mtoto. Unaonaje juu ya mambo kama haya?

Jibu: Ikiwa watoto wanawaudhi waswaliji, kwa kucheza, kupigana, kupiga ukelele na kunyanyua sauti, basi yule ambaye anawaleta nachelea akaja kupata dhambi. Kwa sababu amewashawishi waswaliji na kuwakasirisha[1]. Mwanamke kubaki kwake nyumbani kwake pamoja na watoto wake ni bora kuliko kuja kwake msikitini na hali hii.

Ama ikiwa mazowea ya mtoto ni ya utulivu na mwenye adabu hakuna ubaya kuwaleta. Akianza kufanya cha kufanya basi yule mlezi wake ndiye mwenye jukumu juu ya jambo lake, kumtia sawa na kumtuliza.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/kuleta-watoto-wanaoleta-vurugu-msikitini-wakati-wa-darsa/

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (41) http://binothaimeen.net/content/1618
  • Imechapishwa: 04/10/2018