Kuvaa Utaji Kwa Ajili Ya Kukosa Idhini Ya Hajj

Swali: Kuna mtu amekosa rukhusa ya hajj na kwa ajili hiyo akavaa mavazi ya kawaida baada ya Ihraam ili kuwakwepa polisi. Je, ni lazima kwake kutoa fidia? Ni ipi hukumu ya kukusudia kutumbukia kwenye dhambi kama hii?

Jibu: Kitendo hichi kina dhambi mbili:

1- Kumuasi mtawala ambaye hakuruhusu kuhiji bila ya rukhusa kwa ajili ya amani na kuwapa nafasi ya kutosha mahujaji.

2- Amevaa nguo za kushonwa wakati wa Ihraam bila ya kuwepo sababu ya Kishari´ah. Haijuzu kwake kufanya hivi. Ni juu yake kutoa fidia. Ana khiyari ima ya kulisha masikini sita, kuchinja kondoo au kufunga siku tatu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (39) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighasah%20%208%20-%2011%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017