Kutumia sabuni wakati wa kutawadha

Swali: Ni ipi hukumu ya kuosha mikono na uso kwa sabuni wakati wa kutawadha?

Jibu: Kuosha mikono na uso kwa sabuni wakati wa kutawadha sio jambo lililowekwa katika Shari´ah. Bali ni kupetuka mpaka na kupindukia. Imethibiti ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wameangamia wale wenye kuvuka mipaka. Wameangamia wale wenye kuvuka mipaka.”

Alisema hivo mara tatu.

Lau tuseme kuwa kwenye mikono ya mtu kuna uchafu usiotoka isipokuwa kwa kutumia sabuni au kitu kingine kinachosafisha, katika hali hiyo hakuna ubaya. Ama ikiwa ndio mazowea ya mtu basi kutumia sabuni kutazingatiwa kuwa ni kuvuka mipaka na Bid´ah. Mtu asifanye hivo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/151)
  • Imechapishwa: 01/07/2017