Kutofautiana kwa wanachuoni katika kuapa kwa talaka

Swali: Ni yapi maoni yako kwa watu ambao daima wanaapa Talaka kwenye ndimi zao, kwa kusema: “Ni juu yangu Talaka nikitimiza.” Na huenda akatimiza hilo na wakati mwingine huenda asitimize. Je, kwa hilo Talaka hupita?

Jibu: Akinuia kupita, inapita kwa Ijmaa´. Ama akinuia yamini; kama kufanya, kuhimiza au kukataza kitu, hapa wametofautiana wanachuoni na wengi wao wanaona kuwa inapita. Na kuna kundi linalosema kuwa haipiti, akiwemo Shaykh-ul-Slaam na wengineo wanaona hukumu yake ni kama ya yamini. Atatoa kafara ya yamini.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2913
  • Imechapishwa: 28/02/2018