Kutoa swadaqah nguo zilizochanikachanika

Swali: Umesema kuwa mtu inafaa kwa mtu kutoa swadaqah mavazi yaliyoraruka. Je, haya yanapingana na maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

وَلَا تَيَمَّمُوا الْخَبِيثَ مِنْهُ تُنفِقُونَ وَلَسْتُم بِآخِذِيهِ إِلَّا أَن تُغْمِضُوا فِيهِ

”Na wala msikusudie vibaya kutoka humo mkavitoa ilihali nyinyi wenyewe si wenye kuvichukuwa isipokuwa kuvifumbia macho.”[1]

Jibu: Hayapingani. Kwa sababu Aayah inazungumzia zakaah. Haijuzu kwa mtu akakusudia kutoa ile mali yake ile mbaya katika zakaah. Ama kuhusu kile ambacho sio wajibu kwake kukitoa, anaweza kutoa kile anachokitaka. Hapana shaka kwamba kutoa swadaqah kitu hichi ni bora kuliko kukiharibu.

[1] 02:267

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (56) http://binothaimeen.net/content/1271
  • Imechapishwa: 19/05/2020