Kutoa pole kwa familia ya mtenda maasi


Swali: Wakati fulani inatokea mtu kufa ima kwa kujiua mwenyewe, mlevi ambaye amekunywa kilevi kilicho na kiwango kikubwa cha sukari kinachompelekea kufa au mtu mwenye kumshambulia kwa ajili ya kumaliza uovu wake. Je, inafaa kumfajiri mzazi wa huyo mfiliwa kwa moja miongoni mwa sababu hizi au nyenginezo? Kwa sababu nasita mara nyingi kama nende au nisende?

Jibu: Hakuna neno kutoa pole. Bali imependekezwa ijapokuwa aliyekufa ni kwa ajili ya kujiua mwenyewe au sababu nyenginezo. Ni kama ambavyo imependekezwa kuwapa pole familia ya ambaye ameuliwa kwa ajili ya kulipizwa kisasi au kufanyiwa adhabu kama mfano wa mzinzi ambaye tayari kishaingia ndani ya ndoa. Vivyo hivyo yule mwenye kunywa kilevi mpaka akafa kwa sababu hiyo. Hakuna ubaya kuwapa pole familia yake na wala hakuna ubaya kumuombea yeye du´aa ya msamaha na rehema na watu mfano wake. Mtu huyu ataoshwa na kuswaliwa. Lakini waislamu maalum, kama mfano wa mfalme, Qaadhiy na watu mfano wake, wasimswalie. Bali aswaliwe na baadhi ya watu kwa ajili ya kuwafanya wengine kukikimbia hicho kitendo chake kiovu.

Kuhusu yule ambaye anakufa kwa sababu ya wengine kumshambulia mtu huyo amedhulumiwa na anatakiwa kuswaliwa na kuombewa du´aa akiwa ni muislamu. Vivyo hivyo anayekufa kwa ajili ya kulipizwa kisasi, kama tulivyotangulia kutaja. Mtu huyu anatakiwa kuswaliwa, kuombewa du´aa na kupewa pole familia yake katika juu ya jambo hilo akiwa ni muislamu na hakufanya kitu chenye kumpelekea kuritadi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (04/226)
  • Imechapishwa: 18/02/2020