Swali: Mama yangu alilipa fidia ya swawm juu ya vipindi mbalimbali; mwanzoni mwa mwezi, katikati yake na mwishoni mwake ambapo akatimiza siku thelathini. Je, kitendo chake ni sahihi?

Jibu: Ndio. Kitendo chake ni sahihi. Lakini kuzidisha kwake siku moja katika  mwaka huu… kwani mwezi huu tulitimiza siku thelathini au hatukutimiza? Ile siku ya ziada aliyozidisha chakula itazingatiwa kuwa ni swadaqah na wala haitohesabika kuwa ni kafara juu ya swawm. Kwa sababu mwaka huu mwezi [wa Ramadhaan] ulikuwa siku ishirini na tisa.

Kutofautisha hakuna neno. Kwa mfano baada ya kupita siku kumi mtu anaweza kutoa kafara. Kukipita siku kumi zengine akatoa. Mwishoni mwa mwezi akatoa kile kilichobaki. Hakuna kizuizi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (43) http://binothaimeen.net/content/984
  • Imechapishwa: 12/01/2019