Kuswali Rak´ah mbili za kufika kutoka safarini nyumbani?

Swali: Kuswali Rak´ah mbili pindi mtu amefika kutoka safarini ni miongoni mwa zile swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu? Je, ziswaliwe wakati ambapo imekatazwa kuswali ndani yake? Mtu anayeziswali nyumbani ameafiki Sunnah au ni lazima kuziswali msikitini peke yake?

Jibu: Sunnah ni yeye aziswali msikitini pale anapofika. Akusudie moja ya misikiti na aswali Rak´ah mbili. Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa ni kwamba zikikutana na wakati wa baada ya alasiri basi ni miongoni mwa swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifika wakati wa asubuhi baada ya jua kuchomoza. Akifika wakati huo, wakati wa usiku au wakati wa adhuhuri ndio bora zaidi. Ikiwa hakuna wepesi kufika wakati mwingine isipokuwa tu baada ya alasiri, basi kinachodhihiri ni kwamba ni miongoni mwa swalah zinazoswaliwa kutokana na sababu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6688/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9-%D8%B1%D9%83%D8%B9%D8%AA%D9%8A%D9%86-%D8%B9%D9%86%D8%AF-%D8%A7%D9%84%D9%82%D8%AF%D9%88%D9%85-%D9%85%D9%86-%D8%A7%D9%84%D8%B3%D9%81%D8%B1
  • Imechapishwa: 25/12/2020