Kusujudu kwenye ncha ya kilemba au kofia

Swali: Je, inafaa kwa mtu pindi anapotaka kusujudu ndani ya swalah akaweka ncha ya kilemba chake mahali pa kusujudia ili asujudu juu yake?

Jibu: Haitakikani kufanya hivi isipokuwa wakati wa haja. Kwa mfano mahali hapo kuna joto au baridi kali. Ni kama ambavo Maswahabah walivokuwa wakisujudu katika ncha ya nguo zao wakati ambapo ardhi ni yenye joto kali, yenye baridi au kuna kokoto. Lakini ikiwa ni pasi na haja haitakikani kufanya hivo. Bali anatakiwa kusujudu juu ya ardhi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 14/02/2021