Kusoma ndani ya msahafu katika Fajr


Swali: Inajuzu kuswali ndani ya msahafu katika swalah za faradhi na khaswa katika swalah ya Fajr?

Jibu: Swalah ya Fajr imejengeka juu ya uwepesishaji. Mtu anatakiwa kusoma kutoka kichwani mwake kile kitachomkuia chepesi ijapo ni katika zile Suurah fupifupi. Akiwa ni imamu basi ahifadhi baadhi ya Suurah za kati na kati na pia ahifadhi Suurah “as-Sajdah” na “al-Insaan” ili aweze kuzisoma Fajr ya siku ya ijumaa. Kusoma ndani ya msahafu inakuwa katika swalah ya usiku au swalah ya Tarawiyh.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 27/02/2021