Kusoma kwa sauti katika swalah za siri


Swali: Je, inajuzu kusoma kwa sauti katika Swalah za kusomwa kwa siri?

Jibu: Kujuzu inajuzu, lakini kusoma kwa siri ni bora. Wakati fulani alikuwa akisoma kwa sauti, anasoma kwa sauti Aayah. Lakini mara nyingi, alikuwa akisoma kwa siri (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Hii ndio Sunnah. Alikuwa akisoma kwa siri kama katika Swalah ya Dhuhr na ´Aswr, lakini kusoma kwa sauti katika baadhi ya nyakati, hivi ndio bora.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 24/03/2018