Kushuka kwa Allaah usiku wa nusu ya Sha´baan kupitia upokezi wa Kathiyr bin Murrah al-Hadhwramiy 03

84 – Ahmad bin Muhammad bin Yuusuf ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Ziyaad: al-Hasan bin ´Aliy bin Shabiyb ametuhadithia: Nilimsikia Muhammad bin Khalaf al-´Asqalaaniy akisema: Muhammad bin Yuusuf ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Thawbaan, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Makh-uul, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, kutoka kwa Kathiyr bin Murrah ambaye amesema:

“Kila usiku wa nusu Sha´baan Allaah (´Azza wa Jall) huwatazama watu wa ardhini ambapo akawasamehe isipokuwa mshirikina au mwenye chuki.”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 166
  • Imechapishwa: 09/05/2020
  • taaliki: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy