Kushuka kwa Allaah siku ya ´Arafah kupitia upokezi wa Umm Salamah


95- Abu Bakr an-Naysaabuuriy ametuhadithia: Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: Shujaa´ bin al-Waliyd ametuhadithia: Nimemsikia Sulaymaan bin Mahraan, kutoka kwa Abu Swaalih aliyesimulia kuwa Umm Salamah amesema:

“Uzuri ulioje wa siku ambayo Allaah (´Azza wa Jall) hushuka katika mbingu ya chini ya dunia. Kukasemwa: “Ni siku gani hiyo?” Akasema: “Ni siku ya ´Arafah.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 174
  • Imechapishwa: 14/01/2021