51 – Muhammad bin Sahl ametuhadithia: Muhammad bin Yuusuf bin Sa´d ametuhadithia: Usayd bin ´Aaswim ametuhadithia: ´Aamir bin Ibraahiym al-Aswbahaaniy ametuhadithia: Ya´quub bin ´Abdillaah at-Tamiymiy ametuhadithia, kutoka kwa Abu Rib´iy, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Swaalih, kutoka kwa Abu Hurayrah ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) hushuka kwenye mbingu ya dunia katika ile theluthi yenye kubaki ya mwisho na anasema: ”Je, kuna mwenye kuomba msamaha nimsamehe? Je, kuna mwenye kuomba nimpe? Je, kuna mgonjwa nimponye?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 129-130
  • Imechapishwa: 10/03/2020