34- Abu Muhammad bin Swaa´id ametukhabarisha: Muhammad bin Ishaaq ametuhadithia: ´Abdullaah bin Swaalih Abu Swaalih ametuhadithia: al-Hiql bin Ziyaad amenihadithia, kutoka kwa as-Sadafiy: az-Zuhriy amenihadithia: Abu Salamah ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu ´Abdillaah al-Agharr, Swahibah wa Abu Hurayrah, wamenihadithia kwamba Abu Hurayrah amemweleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku pindi kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku katika mbingu ya dunia na husema mpaka alfajiri inaingia: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe? Ni nani mwenye kiniomba nimpe?”

´Abdullaah bin Ziyaad bin Sam´aan pia ameipokea kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa al-Agharr peke yake, kutoka kwa Abu Hurayrah.

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 117-118
  • Imechapishwa: 16/01/2020