Kuhusiana na Hadiyth kupitia kwa Bishr bin ´Umar kutoka kwa Maalik, ameeleza:

27- Abu ´Aliy al-Maalikiy Muhammad bin Sulaymaan al-Qaadhwiy ametuhadithia Baswrah: Bundaar ametuhadithia…

Abu Bakr an-Naysaabuuriy pia ametuhadithia: Muhammad bin Yahyaa ametuhadithia …

Vilevile Ahmad bin Kaamil ametuhadithia: Abu Qilaabah ametuhadithia …

Wamesema: Bishr bin ´Umar ametuhadithia: Maalik ametuhadithia …

Vilevile ´Ubaydullâh bin ´Abdis-Swamad bin al-Muhtadiy na Muhammad bin Badr ametuhadithia: Bakr bin Sahl ametuhadithia: ´Abdullaah bin Yuusuf ametuhadithia: Maalik ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Shihaab, kutoka kwa ´Abdullaah al-Agharr, kutoka kwa Abu Hurayrah aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mola wetu (´Azza wa Jall) hushuka kila usiku katika mbingu ya chini ya dunia kunapobaki theluthi ya mwisho ya usiku na anasema: “Ni nani mwenye kuniomba nimuitikie? Ni nani mwenye kunitaka kitu nimpe? Ni nani aniombae maghfirah nimghufurie?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 110-112
  • Imechapishwa: 02/01/2020