Kushuka kwa Allaah kupitia upokezi wa ´Abdullaah bin Mas´uud 3

10- ´Abdullaah bin Muhammad bin Ziyaad ametuhadithia: Abu Umayyah na Muhammad bin ´Abdil-Malik amenihadithia: Ja´far bin ´Awn ametuhadithia: Ibraahiym al-Hajariy ametuhadithia, kutoka kwa Abul-Ahwas, kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) huifungua milango ya mbingu katika ile theluthi ya usiku wa mwisho uliyobaki. Kisha Anashuka katika mbingu ya dunia ambapo anaikunjua mikono Yake na kusema mpaka alfajiri inaingia: “Hakuna mja mwenye kuniomba nimpe?”

Ja´far hakuirufaisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-un-Nuzuul, uk. 99
  • Imechapishwa: 15/01/2018