Kusherehekea maulidi ni ada au ´ibaadah?


Swali: Wako wanaosema kwamba kusherehekea maulidi ni katika ada na sio ´ibaadah?

Jibu: Mtu anafanya kitendo hichi na hataki thawabu zozote, kujikurubisha kwa Allaah na wala hataki kitu chochote? Haya ndio malengo ya wale washerehekeaji? Kwa msemo mwingine ni kwamba hawatarajii kupata kheri yoyote kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa sababu ya kitendo hichi? Ni vipi inakuwa hivo? Wale wanaofanya mambo haya wanaamini kuwa jambo hili ni haki, jambo zuri na kwamba wanajikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa jambo hilo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bid´at-ul-Mawaalid wa mahabbat-in-Nabiyy http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=36078
  • Imechapishwa: 08/11/2019