Swali: Je, ni sahihi kwamba haifai kurusha vijiwe ambavyo tayari vimeshatumiwa kwenye nguzo?

Jibu: Hapana, si sahihi. Ukipata vijiwe ardhini, hata kama ni kwa ndani ya ukuta, viokote na uvirushe. Hakuna dalili inayosema kua havirushwi. Hata hivyo haifai kwenda kuleta vijiwe kutoka ndani ya ukuta ukavirusha.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 04/04/2020