Kupiga dufu bila ya kipaza sauti wala redio

Swali: Ni ipi hukumu ya kupiga dufu wakati wa harusi?

Jibu: Haina neno. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) aliamrisha hilo. Aliamrisha wanawake kupiga dufu ili ndoa iweze kujulikana. Imependekezwa kwa wanawake kupiga dufu katika mazingira ya kike na wawe wao kwa wao. Hata hivyo haitakiwi kuimba kwenye kipaza sauti au kusikilizwa kwenye redio. Inatakiwa iwe sauti za wanawake tu miongoni mwao. Haina neno. Ni njia ya kutangaza ndoa na ni katika Sunnah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta’mmulaat fiy Aakhir Suurat-il-Ahzaab, uk. 427
  • Imechapishwa: 21/09/2020