Kupeana damu na kupoteza damu nyingi wakati wa swawm


Swali: Je, kuchotwa damu nyingi ya kupeana kunamfunguza mwenye kufunga?

Jibu: Kuchotwa damu nyingi ya kupeana ikiwa kunapelekea katika yale yanayopelekea chuku ambapo ni kudhoofika kwa mwili kwa yule mgonjwa na hivyo akahitajia chakula, basi kutakuwa na hukumu moja kama ya kuumika. Ama kile kiwango kikubwa cha damu kinachotoka pasi na mtu mwenyewe kutaka, kwa mfano mtu akapata majeraha na hivyo akatokwa na damu nyingi,  hiyo haidhuru kwa sababu si kwa matakwa ya mtu mwenyewe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/250)
  • Imechapishwa: 03/05/2021