Kupatwa na hadathi katikati ya wudhuu´


Swali: Nikiosha uchi wangu kisha nikavaa suruwali na katikati ya wudhuu´ nikahisi kupatwa na hadathi, je, nianze wudhuu´ upya?

Jibu: Mtu akiosha uchi wake na akajisafisha halazimiki kurudi kuosha tena uchi mara nyingine isipokuwa akitokwa na kitu. Kujengea juu ya hili muulizaji ikiwa amepatwa na hadathi katikati ya wudhuu´ basi hatorudi tena kuosha tupu yake ikiwa hakutokwa na kitu. Tunakusudia kitu chenye kuhisiwa na si upepo. Si lazima kuosha tupu yake kwa kutokwa na upepo ikiwa hakutokwa na majimaji. Kutokana na hili kama amechengukwa na wudhuu´ kwa upepo wakati wa kutawadha kwake hatorudi kuosha tupu yake. Nakusudia upepo usioambatana na majimaji. Hivyo hatorudi kuosha tupu yake. Kitachompasa ni kurudi kutawadha upya. Nikimaanisha kwamba atarudi aoshe vitanga vyake vya mikono, asukutue, apalizie, aoshe uso wake na kadhalika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (17) http://binothaimeen.net/content/6817
  • Imechapishwa: 14/03/2021