Kuonekana Allaah duniani na Aakhirah ni jambo lenye kujuzu


al-Khaliyliy amesema:

“Kumetokea mgororo mkubwa baina ya mapote ya Ummah juu ya uwezekano wa kumuona Allaah na kutokea kwake. Kundi linalojinasibisha na Sunnah kwa jina Salafiyyah, Ashaa´irah, Maaturiydiyyah, Dhwaahiriyyah na wengine wanasema kuwa ni jambo linalowezekana hapa duniani na Aakhirah. Pamoja na kuwa wengi jamhuri wanaonelea litatokea Aakhirah na si duniani.”

Akaendelea kusema:

“Kuna kundi limeonelea kuwa ni jambo linaweza kutokea duniani na Aakhirah.”

Kisha baada ya hapo akanukuu maoni ya Suufiyyah juu ya hilo.

Madhehebu ya Salaf, Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanathibitisha waumini kumuona Mola wao Peponi kutokana na dalili za wazi kabisa kutoka katika Qur-aan na Sunnah juu ya hilo ambazo punde tu tutaziorodhesha.

Kuhusu Allaah kuonekana duniani ni jambo lenye kujuzu. Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawezi kuomba kitu kisichojuzu. Pamoja na hivyo halikutokea kwa kuwa viumbe hawawezi kustahamili hilo kutokana na udhaifu wao. Mlima ulisagika. Vipi kuhusu mwanaadamu? Kuhusu Aakhirah ni jambo lenye kujuzu na litalotokea kwa waumini kwa kuwa Allaah atawafanya kuwa na nguvu na atawawezesha hilo kwa ajili ya kuwakirimu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 48
  • Imechapishwa: 14/01/2017