Swali: Mswaliji akisoma maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Mtume. Hivyo enyi walioamini mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (33:56)

akapita katika Aayah ya Istighfaar au mengineyo aitamke ndani ya swalah au aombe Istighfaar?

Jibu: Hayo yamependekezwa katika swalah ya sunnah kama vile kisimamo cha usiku. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali Tahajjud usiku ambapo anaposoma Aayah ya rehema anaiomba, anapopita katika Aayah ya kinga anajikinga na anapopita katika Aayah ya Tasbiyh anasabihi. Allaah (Ta´ala) amesema:

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ

“Hakika mna kigezo chema kwa Mtume wa Allaah.” (33:21)

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini kama mlivyoniona nikiswali.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy katika “as-Swahiyh” yake.

[1] al-Bukhaariy (7246) na ad-Daarimiy (1253).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/41)
  • Imechapishwa: 03/06/2018