Kuoga kwa sababu ya jua kali kunamtosheleza mtu na kutawadha?

Swali: Je, kuoga kwa ajili ya kutaka kupata baridi kunatosheleza kutokamana na kutawadha? Ni wudhuu´ gani ambao unatosheleza kutokamana na kutawadha?

Jibu: Kuoga kwa ajili ya kutaka kupata baridi hakutoshelezi kutokamana na kutawadha. Kwa sababu kuoga kunakuwa kwa ajili ya uchafu. Kuoga kwa ajili ya  kutaka kupata baridi hakutokamani na uchafu.

Kuhusu kuoga kwa ajili ya janaba kunamtosheleza mtu na kutawadha. Mtu akiwa na janaba ambapo akaoga na kupalizia na kusukutua na akaosha mwili wake wote basi huko kunamtosheleza na kutia wudhuu´ hata kama hakutawadha. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Tabaarak wa Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا

“Enyi walioamini!  Mnaposimama kwa ajili ya swalah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye visugudi, na panguseni vichwa vyenu na [osheni] miguu yenu hadi kwenye vifundo. Na mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni.” (05:06)

Dalili hapa ni kwamba Allaah ametaja kujisafisha na wala hakutaja wudhuu´. Kujengea juu ya hili kuoga kwa ajili ya janaba kunamtosheleza mtu kutokamana na wudhuu´. Mtu akiwa na janaba ambapo akapalizia na kusukutua na akayaeneza maji juu ya mwili wake, basi aswali na hakuna neno kwake. Kuoga kwa ajili ya kutaka kupata baridi hakutoshelezi.

Muulizaji: Vipi ikiwa atagusa tupu yake?

Jibu: Akigusa tupu yake wudhuu´ wake hauchenguki. Kugusa tupu hakuchengui wudhuu´ isipokuwa ikiwa ni kwa matamanio. Ama akigusa pasi na matamanio akitawadha ndio bora zaidi. Asipofanya hivo hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=uGzmaelIayM
  • Imechapishwa: 14/11/2017