Swali: Mwenye kusema kuwa makafiri ni bora kuliko waislamu inapokuja katika tabia, nidhamu na mikakati. Upande mwingine akawashambulia na kuwatukana waislamu. Sambamba na hilo hawapendi makafiri. Ni ipi hukumu yake?

Jibu: Hawezi kusema kuwa wao ni bora kuliko waislamu isipokuwa ni kwa sababu anawapenda. Hawezi kusema kuwa makafiri ni bora kuliko waislamu isipokuwa ni kwa sababu anawapenda na anapendezwa nao. Kunachelea juu yake kuritadi.

Ni kweli kwamba waislamu wanaweza kuwa wamefanya upungufu katika baadhi ya mambo, haya hutokea. Waislamu wakafanya upungufu katika mambo ambayo ni wajibu kwao kuyatilia umuhimu. Ni jambo hutokea na hatulipingi. Sambamba na hilo makafiri wakawa wametangulia mbele katika mambo ya viwanda, uvumbuzi na kuyapanga mambo ya dunia yao. Hapana shaka ya kwamba wamebobea katika mambo haya. Lakini hata hivyo haya hayapelekei kwamba wao ni bora kuliko waislamu kwa hali yoyote. Waislamu ni bora kuliko makafiri vovyote waislamu watavyokuwa na mapungufu. Waislamu wako na Uislamu na wale wengine wako na ukafiri. Hivyo waislamu ni bora kuliko makafiri kwa hali yoyote ile.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunanjia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidhl-il-Islaam (08) http://ajurry.com/safrawy/chorohat-elakida/chorohat-nawakid-elislam/charh-salah-fawzan/08.mp3
  • Imechapishwa: 12/02/2019