Kumwita jina la Malaika mtoto wa kike na jina la Bayaan

Swali: Ni ipi hukumu ya kumpanga jina “Bayaan” mtoto wa kike?

Jibu: Kimsingi ni kufaa isipokuwa katika yale ambayo dalili imejulisha kuwa ni haramu, majina maalum kwa wanamme au majina maalum kwa wanawake. Mfano kumwita mtoto wa kike Malaak, ni kitu kisichofaa. Kwa sababu ni lugha yenye manaa ya mfalme. Sababu nyingine kufanya hivo ni katika kumwita mfalme kwa dhamira ya kike. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ لَيُسَمُّونَ الْمَلَائِكَةَ تَسْمِيَةَ الْأُنثَىٰ

“Hakika wale amabo hawaamini Aakhirah bila shaka wanawaita Malaika kwa majina ya kike.”[1]

[1] 53:27

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
  • Imechapishwa: 05/06/2020