Kumwambia kafiri ´asante`


Swali: Inajuzu kumwambia baadhi ya matamshi yule kafiri aliyekufanyia mema fulani kama ”asante” au ”ujazwe kheri”?

Jibu: Ndio, haya yanaingia katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yule mwenye kukufanyieni wema basi mlipeni. Msipokuwa na chakumlipa, basi muombeeni du´aa mpaka muhisi kuwa mmemlipa.”

Ikiwa kuna ambaye sio muislamu atakufanyia wema, basi na wewe mlipe. Hii ni tabia moja wapo ya Uislamu. Pengine kufanya hiv kukaulainisha moyo wake na matokeo yake akawapenda waislamu na akaingia katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/683
  • Imechapishwa: 18/10/2017