Kumuomba mtu kwa haki au kwa uso wake


Swali: Ni sahihi mtu akamuomba mwengine kwa uso wake?

Jibu: Ikiwa kuomba ni kupitia mtu hakuna neno. Lakini haifai kumuomba mtu kwa uso wa Allaah. Kwa mfano mtu akasema “Nakuomba kwa haki ya baba yako au kwa uso wa baba yako” hakuna neno. Kama ambavo ´Abdullaah bin Ja´far alivyokuwa akisema kumwambia ami yake ´Aliy bin Abiy Twaalib akimuomba kwa haki ya Ja´far[1] bi maana akimuomba kwa kuunga udugu. Ama Allaah haombwi kwa hilo. Bali inatakiwa kumuomba Allaah kwa majina Yake mazuri, kwa kumwamini au kwa kumpenda kwako.

[1] at-Twabaraaniy (02/1476).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 73
  • Imechapishwa: 22/07/2019